Jumapili 23 Novemba 2025 - 23:10
Jawabu kwa Shubha ya Kihistoria: Je, ni Kweli Nyumba ya Bibi Zahraa (a.s) Ilichomwa Moto?

Hawza/ Katika kipindi kilichoandaliwa huku akihudhuria Hujjatul-Islam Muhammadi Shahroudi, palisisitizwa juu ya kupata maarifa ya Fatimiyyah kama ufunguo wa kufumbua fumbo la historia, na kuchambua shubha muhimu za kihistoria, likiwemo tukio la uvamizi wa nyumba ya Bibi Zahraa (a.s).

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza, katika siku za maombolezo ya Bibi wa walimwengu wawili, Fatimah Zahraa (amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), na kwa madhumuni ya kubainisha pande mbalimbali za historia ya mwanzo wa Uislamu na kujibu maswali ya kihistoria ya wasomi na wapenzi wa Ahlul-Bayt (s.a.w.w), maandishi kamili ya mazungumzo ya kitaalamu kupitia Radio, katika kipindi maalumu cha pamoja na Hujjatul-Islam wal-Muslimin Reza Muhammadi Shahroudi yameletwa kwenu kama ifuatavyo:

“Nataka hifadha kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, na rehema za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na Aali zake watoharifu.

Nawasilisha salamu na heshima kwa marafiki wote wapendwa, pamoja na kutoa rambirambi na pole kwa mnasaba wa siku za shahada ya Bibi mtukufu, Fatimah Zahraa (a.s).

Umuhimu wa Kupata Maarifa ya Fatimiyyah

Hakika jambo muhimu zaidi kwetu ni kupata “maarifa ya Fatimah Zahraa (a.s)”. Tukipata maarifa haya, thamani ya usiku mmoja kwetu itakuwa zaidi ya usiku elfu thelathini. Imam Swadiq (a.s) anasema:

“Yeyote atakayemjua Fatimah kwa haki ya kumjua kwake, basi hakika ameuifikia usiku wa Cheo.”

Mtume Mtukufu (s.a.w.w) pia amesema: “Hakika usiku wa Cheo ni bora kuliko miezi elfu moja.” Hivyo basi, kumjua Bibi Zahraa (a.s) ni sawa na kuufikia usiku wa Cheo—usiku ambao ni siri miongoni mwa siri za Mwenyezi Mungu.

Sisi tunaamini kwamba Bibi Zahraa (a.s) hakujulikana ipasavyo kama inavyotakiwa. Lau angelijulikana vyema wakati wa uhai wake, yale matukio na vipindi vya majonzi vya historia visingalitokea. Cha kusikitisha ni kwamba hadi leo, Waislamu wengi hawajakifahamu cheo kikubwa na hadhi tukufu ya bibi huyu.

Iwapo hata sehemu ndogo tu ya sira yake ya kielimu na kiibada ingelieleweka — kwa mfano kwamba Hasan al-Basri alimwona Bibi Zahraa (a.s) kuwa ndiye mcha Mungu zaidi katika umma, na kwamba imepokewa kuwa alikuwa akiinuka kwa ajili ya swala na ibada kiasi cha kwamba miguu yake mitukufu inavimba — basi shubha nyingi na maswali yasingeibuka.

Shubha zilizotolewa ni hizi: “Je, tukio la kuchomwa moto mlango wa nyumba ya Bibi Zahraa (a.s), na uwepo wake nyuma ya mlango, ni sahihi?”

Na pia wametoa shubha kwamba: Kwa kuwa Imam Ali (a.s) alikuwa ndani ya nyumba, kwa nini Bibi Zahraa (a.s) ndie aliekwenda kufungua mlango?

Hata wamefikia kusema kuwa katika utamaduni wa Kiarabu wa wakati ule, si kawaida mwanamke kufungua mlango, au kwamba nyumba hazikuwa na milango bali zilikuwa zikitenganishwa kwa pazia au mkeka tu.

Katika kujibu, tunasema:

Hapana, hakuna madai kati ya haya yaliyosemwa kuwa hayakuwa na mlango wala wanawake hawafungui mlango yaliyo sahihi. Lakini kuhusu kuchomwa kwa mlango wa nyumba, lazima nisistize kuwa tukio hili ni sahihi.

Unapotaka kutoa maoni juu ya taaluma fulani, lazima utumie mbinu za taaluma hiyo. Huwezi kuitazama historia kwa mantiki za kiakili pekee; kwa sababu kazi ya akili ni kufahamu dhana na mambo ya jumla, si kuchunguza matukio na vielelezo vya kihistoria. Kila taaluma ina mada yake mahsusi, na masuala ya kihistoria yanapaswa kuchambuliwa kwa njia ya kitaaluma ya kihistoria kupitia uchunguzi wa vielelezo na vyanzo.

Kwa njia hii, tunapochunguza vyanzo vya kihistoria, tunaona kwamba tukio hili si tu limeripotiwa katika vyanzo vya Kishia, bali hata katika vyanzo sahihi na mashuhuri vya Kisunni, kwa upana mkubwa, hadi limefikia kiwango cha mutawatir (riwaya nyingi mno zisizoweza kukadhibishwa).

Mtu akifanya uchunguzi wa mtandaoni au kupitia makala za kitaalamu, atayaona madhihirisho ya vielelezo vya tukio hili waziwazi.

Kwa hiyo, njia sahihi ni kuikamata haki ya kihistoria kwa kuchunguza vielelezo, si kwa kutumia uchambuzi wa kiakili usio na msingi. Hatimaye, tukio hili bila shaka lilitokea.

Kwa anayehitaji maelezo zaidi, napendekeza kitabu “Dar Saahil al-Haqiqa”, na pia kitabu changu cha zamani “Pindarha wa Pasokhha (Fikra na Majibu)”, ambavyo ndani yake vielelezo vya tukio hili vimeletwa kwa kinagaubaga. Vitabu hivi vinapatikana pia kwenye mitandao.

Kuhusu swali kwamba: “Kwa nini Bibi Zahraa (a.s) alienda nyuma ya mlango?”

Swali hili limejengeka juu ya dhana potofu.

Wanaoweka shubha hii wanadhani kuwa hali ilikuwa hivi: Kuna watu walikuja nje ya mlango, wakagonga mlango, na watu wa nyumbani hawakujua ni nani yuko nje. Kisha kulikuwa na majadiliano ndani ya nyumba kuhusu ni nani atokee kufungua mlango — je, Imam Ali (a.s), Bibi Zahraa (a.s), Imam Hasan, Imam Husayn, ama Zubayr au wengine waliokuwapo ndani ya nyumba?

Kisha swali hili ndipo likaibuliwa: “Kwa nini Fatimah (a.s) alitoka?” au “Kwa nini Fiddhah au wengine hawakwenda?”

Kosa ni kudhani kuwa tukio hili lilikuwa ni “kubisha mlango kwa kawaida”. Wakati hali haikuwa kwamba mtu amekuja kubisha mlango na watu wa nyumbani hawajui ni nani yuko nje, kisha wajadiliane nani aende kufungua.

Swali wanalouliza ni hili: “Kwa nini mwanamke ndiye aliyekwenda kufungua mlango? Je, si utamaduni wa Kiarabu kwamba mwanamke hafungui mlango?”

Kauli hii yenyewe ina tatizo; kwa sababu kama mwanamke yuko peke yake nyumbani na mwanamke mwingine yuko nyuma ya mlango, je, kwa sababu hakuna mwanaume ndani ya nyumba, basi hatofungua mlango?!

Zaidi ya hayo, katika utamaduni wa wakati huo, hata hapa kwetu Iran, milango ilikuwa na vidude viwili: kimoja kwa umbo la pete, maalumu kwa wanawake, na chengine kwa umbo la nyundo maalumu kwa wanaume. Kama sauti ya kidude cha wanawake ingesikika, basi mwanamke wa nyumbani ndiye aliyekwenda kufungua. Basi haikuwa kwamba wanaume tu ndio waliojibu mlango.

Hali Halisi ya Tukio Ilikuwa Hivi: Wale watu walikuja nyuma ya mlango na wakapiga kelele kwa sauti ya juu wakisema: “Watu waliopo nyumbani watoke waje kutoa kiapo cha utii kwa khalifa wa Mtume; la sivyo, tutachoma nyumba moto!”

Katika mazingira kama haya, Bibi Zahraa (a.s) alienda mwenyewe nyuma ya mlango ili pengine kwa kuona uwepo wake, wavamizi waheshimu na warudi nyuma. akasema:
“Mimi ndiye Fatimah Zahraa. Hasan na Husayn pia wamo ndani ya nyumba.”

Kwa hiyo, tukio hili halikuwa suala la kubisha mlango tu, bali lilikuwa ni tishio na onyo kubwa. Katika mazingira kama hayo, Bibi Zahraa (a.s) alikwenda kujihatarisha ili kutetea heshima ya nyumba na watu wa Ahlul Bayt.

Alikwenda ili kuzuia ghasia na umwagikaji damu. Aalikwenda ili tukio lisitokee, kwa tumaini kwamba wavamizi wangeona haya na warejee. Hii ndiyo hakika ya tukio.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha